Saturday 13 January 2007

UTANGULIZI

Katika mtiririko wa maelezo yaliyomo ndani ya mtandao,utaelewa tafasiri ya neno TCCIA,TABORA,SACCOS,
na utafahamu taratibu za kujiunga na SACCOS hii pia utaelewa uhalali wa SACCOS kuendesha shughuli zake kwa mujibu wa sheria ya ushirika namba 20 ya mwaka 2003.
Soma maelezo zaidi uelewe wajibu wa SACCOS kwa mwanachama na wajibu wa mwanachama kwa SACCOS.
Hatimaye utafahamu ni wakati gani uanachama wako utakapokoma na mwisho kabisa utafahamu majina ya wajumbe wa Bodi ya uanzilishi wa
TCCIA TABORA SACCOS LTD.

MAANA YA NENO TCCIA TABORA SACCOS.

TCCIA ni kifupi cha neno la kiingereza lenye tafasiri ya kiswahili inayosomeka ifuatavyo,CHAMA CHA WAFANYABIASHARA WENYE VIWANDA NA KILIMO.

TABORA lina maana ya mkoa wa TABORA.

SACCOS ni ufupisho wa neno la kiingereza lenye tafasiri ya kiswahili inayosomeka kuwa CHAMA CHA USHIRIKA CHA AKIBA NA MIKOPO.

TARATIBU NA SIFA ZA KUJIUNGA NA SACCOS.

A. UWE MKAZI WA TABORA MANISPAA.
B. UJIAMINI KWAMBA WEWE NI MWAMINIFU.
C. UWE MFANYABIASHARA,MKULIMA,MWENYE KIWANDA,MFANYAKAZI,KIKUNDI AU TAASISI.
D. FOMU YA MAOMBI YA UANACHAMA TSHS 1,000/=.
E. ADA YA KIINGILIO SHS 10,000/=.
F. HISA TANO T.SHS 50,000/= NI VIZURI UKANUNUA HISA NYINGI KWANI HISA MOJA NI TSHS 10,000/=
G. MTOTO WA UMRI CHINI YA MIAKA 18 ANARUHUSIWA KUWA MWANACHAMA KWA KUSIMAMIWA NA WAZAZI AU WALEZI WAKE.
H. UWE NA AKIBA KATIKA SACCOS.
I. USIWE MTU WA MAJUNGU NA UZUSHI.
J. UWE MWEPESI KUSHIRIKI VIKAO VYA CHAMA PALE UTAKAPOHITAJIKA.
K. UKIACHA UANACHAMA UTAREJESHEWA HISA ZAKO ZOTE.
L. HISA ZINAWEZA KURITHIWA NA KUENDELEZWA NA MRITHI.
M. KILA MWANACHAMA ATAPASWA KUWA NA AKAUNTI KWENYE SACCOS HII.

UHALALI WA KUENDESHA SHUGHULI ZA SACCOS.

Chama hiki kimepata usajili Na. 578 Tarehe 14.02.2006 kwa Mrajisi wa Vyama vya Ushirika chini ya sheria namba 20 ya mwaka 2003 ya Vyama vya Ushirika.

Chama hiki kilisajiriwa baada ya kutimiza masharti yote ikiwa ni pamoja na SERA,KATIBA,UANACHAMA,BODI YA UANZILISHI,ANWANI YA CHAMA NA OFISI YA KUENDESHEA SHUGHULI.

Kwa sasa chama kinayo Akaunti katika Benki ya CRDB, Chama hiki kinayo haki ya kukusanya michango,kuuza hisa na kutoa mikopo kwa wanachama,yote hayo yametimizwa.

Kwa kuzingatia vikao halali vya wanachama waanzilishi chini ya Afisa Ushirika wa Manispaa na Mrajisi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Tabora na uongozi wa CRDB Tawi la Tabora.

OFISI ZA TCCIA TABORA SACCOS LTD.


Kwa sasa ofisi zipo katika jengo la NHC kata ya Gongoni mtaa wa Lumumba, Mkabala na duka la vitabu la TMP Tabora,
Anwani ina maelekezo sahihi,barua zote zitumwe kwa Katibu M/kiti
wa Bodi,Meneja wa SACCOS.

FAIDA ZA KUWA MWANACHAMA WA SACCOS.

Mwanachama baada ya kutimiza wajibu wake kama inavyoelezwa katika kipengele namba 2 cha kijitabu hiki atapata fursa ya kushiriki mikutano ya Chama,kushiriki semina za mafunzo katika kumjengea uelewa zaidi wa taratibu za kutunza akiba na mikopo na atapata fursa ya kukopa.

Ieleweke kwamba mikopo kwa wanachama itatolewa kuzingatia akiba yake ndani ya Chama na ambapo mkopaji atakopeshwa si zaidi ya mara tatu ya akiba yake chamani.

Inawezekana mwanachama akawa na hisa zake ndani ya chama na asihitaji kukopa huyu atapata gawio toka katika faida itakayopatikana kulingana na hisa zake baada ya mahesabu ya mwaka.

AINA YA MIKOPO ITOLEWAYO

-Biashara.
-Kilimo na Mifugo.
-Elimu.
-Maendeleo
-Dharula,jamii.
-Dharula,Biashara
-Mazao makavu (stock)

DHAMANA YA MIKOPO.

Mwanachama atakuwa na haki ya kukopa ama ilivyoelezwa awali isipokuwa lazima adhaminiwe na wanachama wawili,ambao nao wana sifa ya kuwa wakopaji.

Wadhamini hao watamdhamini mkopaji kwa kujaza fomu maalumu iliyoandikwa na Bodi ya SACCOS na kutia sahihi zao.

La muhimu zaidi wadhamini wawe tayarikuhakikisha mkopo unarejeshwa kwa wakati kama ilivyoelezwa katika kipengele namba 5.

Wanachama watapatiwa semina kujua wajibu wao,viongozi watapatiwa semina za kuwajengea haki ipasavyo,ambapo wafanya kazi wa SACCOS watapatiwa mafunzo ya kuendesha shughuli za ki fedha na za ki benki.

Semina na mafunzo hayo yatafadhiliwa na CRDB Benki ltd.

RIBA YA MIKOPO.


Mikopo itatozwa riba ya asilimia ndogo ambayo imefafanuliwa katika sera ya bei,bidhaa na huduma zitakazotolewa na SACCOS hii.

MTAJI WA SACCOS KATIKA KUMUDU KUKOPESHA.

Inashangaza mtu kuweka pesa kidogo na baadae akope pesa mara tatu ya pesa alizowekeza,kwa ujumla mtaji wa kukopesha zaidi tutaupata kutoka kwa m bia wetu ambae ni

Benki ya CRDB LTD,itakuwa tayari kukopesha SACCOS yetu pesa kwa kiwango chochotekwa kuzingatia mahitaji ya wanachama wetu baada ya kukopesha pesa CRDB atakuwa tayari kupokea riba kwa asilimia ndogo ambayo hailingani na asilimia tunazotozwwa kati ya mteja mmoja mmoja na benki,dhamana ya mkopo itakuwa ni wanachama wenyewe.

MUDA WA KUREJESHA.

Mkopaji atawajibisha kurejesha mkopo kwa kuzingatia mkataba na aina ya mkopo,kutakuwa na marejesho ya kidogo kidogo kila
wiki au mwezi,na muda wa kukaa na mkopo utakuwa kati ya mwezi mmoja,miezi 3,miezi 6,na mwaka mmoja.Bodi na kamati ya
mikopo itapendekeza na kufikisha katika mkutano mkuu,hatua za kuchukua mkopaji aliyechelewesha mkopo.

KUMTAMBUA MWANACHAMA.

Kila mwanachama atajaza fomu ya kujiunga na ataweka sahihi katika kitabu cha wanachama na picha yake.Pia atapewa
kitambulisho na kitabu cha fedha.

SALAMU ZA MWENYEKITI WA BODI.

Natumia fursa hii kueleza kwamba SACCOS hii imeanzishwa kwa ridhaa ya Wanachama wa TCCIA na wakazi wa Tabora waliokutana
katika mkutano wa kwanza,na wa pili uliopitisha Katiba tarehe 10.02.2006
Pia ieleweke kwamba kila Mwanachama anayo haki ya kuwa kiongozi wa SACCOS hii,kwa ridhaa ya wanachama,kwa msingi huo
SACCOS hii ni mali ya wanachama wote,kwa mujibu wa Katiba.
Hivyo nia na madhumuni ya SACCOS inaeleweka vizuri ndani ya KATIBA na SERA ambazo zipo katika ofisi za SACCOS,kwa
kifupi lengo kuu ni kumwinua mkazi wa Tabora kimtaji,kiuchumi,ki elimu na maendeleo ya mkoa wetu na kadhalika.

Nawaomba wakazi wa Tabora wajiunge na SACCOS hii ili tujenge misingi imara ya maendeleo ndani ya Tabora.Kwani yote hayo
yaliyofafanuliwa hapo juu yatawezekana kwa kushirikiana.La muhimu zaidi ukikopa tafadhari lipa kwa wakati na katika kujiunga
usisubiri kuhadithiwa.Ukitaka kujua uhondo wa ngoma ingia ucheze.

VIONGOZI WA BODI YA SACCOS.

1. WILLIAM MASUBI -MWENYEKITI WA BODI
2. DICK MULIMUKA -MAKAMU MWENYEKITI WA BODI
3. JOHN L.MCHELE -MWENYEKITI BODI YA MIKOPO
4. MARY D.MANYANGA-MJUMBE WA BODI
5. FRANK MGONJA -MJUMBE WA BODI
6. ZAKAYO MAGANGA -MJUMBE WA BODI
7. MICHAEL MAMBO -MJUMBE WA BODI
8. GULAM H.DEWJI -MJUMBE WA BODI
9. PETRONELA LYIMO-MJUMBE WA BODI

KAMATI YA USIMAMIZI.

1. PAUL B.MATOBOGOLO
2. AMANI MRISHO MAKUNGU
3. ANDREW KISHIKI

MENEJA WA SACCOS.
LAURENCE B. KASALA.

TIMIZA WAJIBU TABORA YENYE NEEMA INAWEZEKANA

ANWANI KAMILI.
TCCIA TABORA SACCOS LIMITED
LUMUMBA STREET
S.L.P 658 SIMU 026 260 4169
REG NO. 578
BARUA PEPE (E-MAIL) tcciatabora@yahoo.co.uk
TOVUTI (WEBSITE) http://tabora-saccos-ltd.blogspot.com
TABORA-TANZANIA